Sisi, viongozi wa dini pamoja na taasisi zinazosimamia mchakato wa uchaguzi
(NEC, TAKUKURU, Polisi pamoja na Msajili wa vyama vya siasa) tuliokutana
leo tarehe 17/9/2015, tumepata nafasi ya kujadili kwa kina suala la uhuru,haki na
amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika 25/10/2015 na wajibu wa kila mdau
kuhakikisha kuwa uhuru,haki na amani vinalindwa kipindi hiki.Suala la uhuru haki
na amani ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini na watanzania wote kwa ujumla na
halina mjadala.Kila mmoja achukuwe nafasi yake kulinda uhuru,haki na amani na
kuweka uzalendo kwanza kuliko kutanguliza maslahi binafsi ya vyama vya siasa.
Viongozi wa dini wamepata nafasi ya kujadili na vyombo hivi masuala ya msingi
kama kuhakikisha kuwa maadili ya uchaguzi yanazingatiwa kwa wote, muda wa
kutangaza matokeo ya kura unazingatiwa , haki ya wananchi kupata matokeo
haraka ili kuepuka fujo wakati wa kusubiri na kutangazwa kwa matokeo. Jeshi la
polisi kutokutumia nguvu kupita kiasi, wajibu wa Msajili kuhakikisha vyama vyote
vinapata fursa sawa na pia tumejadili suala la kutumia nyumba za ibada kama
sehemu ya jukwaa la siasa.
Viongozi wa dini tumekubaliana kwa pamoja kuepuka kutumia nyumba za ibada
kuonyesha ushabiki wa aina yoyote kwa chama chochote cha siasa.
Baada ya kujadili kwa kina masuala hayo viongozi wa dini wanatoa wito ufuatao;
1. Vyombo vya habari vifanye kazi kwa ueledi bila upendeleo na pia kuhakikisha
kuwa inatoa taarifa ya kutosha kuelimisha umma.
2. Tunaishauri NEC kwenye chaguzi zijazo iweke utaratibu maalum wa kuruhusu
wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha pamoja na watu wote
waliojiandikisha/watakaojiandikisha waweze kupiga kura.
3. Tunaishauri NEC
ibada.
kwenye chaguzi zijazo siku ya kupiga kura isiwe siku ya
1
4. NEC iendelee kutoa elimu ya uraia kuhusu haki ya raia kupiga kura na haki yao
ya kukaa mita mia moja kusubiri matokeo yatangazwe kwa utulivu kama ambavyo
NEC imehakikishia viongozi wa dini kuwa kila kituo itabandika matokeo yote
(Urais,Ubunge na Udiwani)
5. Pamoja na kutimiza wajibu wake wa msingi wa kulinda raia na mali zao Jeshi la
polisi wakati huu wa uchaguzi liendelee kutimiza wajibu wake wa kusimamia
amani na taratibu kwa haki bila upendeleo.
6. Wagombea,wafuasi na wanaowanadi, wanaaswa waache mara moja lugha za
matusi,vitisho,kejeli na kukashifiana vinavyoweza kuchochea fujo na kuleta
uvunjifu wa amani wajikite kunadi sera za vyama vyao.
7.Tunawahimiza wananchi kuwa makini katika kufuatilia kampeni na sera
mbalimbali za wagombea, kuzipima kwa hali ya juu sera hizo, kutokuuza kadi zao
za kupigia kura, kutokununuliwa na kujitokeza kwa wingi kutumia uhuru na haki
yao ya kuchagua viongozi wanao wataka kwa hiari na amani.
8. Viongozi wa dini wanawahimiza Watanzania wote kuendelea kuombea nchi hii
kuendelea kuwa taifa lililojengwa katika misingi ya uhuru , haki na amani.
9. Viongozi wa dini tutabaki kuwa manabii na wahubiri wa uhuru,haki na amani
wakati huu , wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi
Sisi viongozi wa dini Tunawashukuru Inspekta generali wa polisi, Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya siasa na Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU kwa ufafanuzi makini na wa kina juu ya nafasi na utayari wao wa
kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha uhuru, haki na amani vinaendelea
nchini.Maelezo yao na mafafanuzi yao tumeyasikia na tutaendeleza kwa kuwa
hiki ni kikao cha mwanzo na tutaendelea kuwa na vikao vingine pamoja nao
kuelekea uchaguzi mkuu ili kufuatilia utekelezaji na kuendeleza makubaliano yetu
katika kuhakikisha uhuru,haki na amani.
Your Ad Spot
Sep 17, 2015
Home
Unlabelled
TAMKO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU UHURU, HAKI NA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
TAMKO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU UHURU, HAKI NA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269