Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi wa mjini Kibondo kwenye uwanja wa Taifa katika
mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo na kuhudhuriwa na Malefu ya
wananchi mkoani Kigoma.
Dk. John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi wakati akiomba kura katika kijiji cha Mnanila
wilayani Buhigwe mkoani Kigoma Dk. Magufuli amesema serikali yake
itaendeleza uhusiano wa Kidiplomasia na mataifa na nchi
mbalimbali pamoja na nchi majirani zinazoshirikiana na Tanzania katika
nyanja za Uchumi, Utamaduni na Siasa.
Ameongeza kwamba ni muhimu
kuendeleza ushirikiano ambao umejengwa na marais wetu wastaafu
waliopita na kusaidia kukuza uchumi wa wananchi wetu katika nchi zetu
ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uchumi wa wananchi wa mataifa haya
unakuwa kutokana na ushirikiano wa biashara na masuala mbalimbali ya
kisiasa na kiutamaduni. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE.KIBONDO)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi katika kijiji cha Mnamila
wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Umati wa Wananchi waliohudhuria katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Taifa mjini Kibondo jioni ya leo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akipanda jukwaani tayari kwa kuwahutubia wananchi kwenye uwanja wa
Taifa mjini Kibondo leo.
Kada wa CCM Bw. Jamal Abdallah
Tamim akipigia debe Mgombea ubunge wa jimbo la Muhambwe
Injinia Atashasta Nditiye katika mkutano huo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo la Muhambwe Injinia Atashasta Nditiye.
Baadhi ya wananchi wakisubiri
msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia
Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli upite huku mabasi pia yakiwa
yameegeshwa kando ya barabara.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akiwasili kwenye uwanja wa Taifa mjini Kibondo tayari kwa kuwahutubia
wananchi mjini Kibondo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akiwanadi wagembea ubunge wa Kasulu Daniel Nsazugwako kulia na Agustino
Zuma Ole katikati.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
awahutubia wananchi wa Kasulu katika mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye uwanja wa Umoja.
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza
wakati msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli ukisubiriwa kuwasili
kwenye uwanja wa Umoja mjini Kasulu.
Kila mahali ni picha za Magufuli tu.
Akina mama wakifurahia hotuba ya Dk. John Pombe Magufuli mjini Buhigwe.
Mama huyu akimfurahia Dk. John
Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwasalimia wananchi akiwa njiani
kuelekea mjini Kasulu huku akiwa amebeba mkungu wa ndizi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akihutubia wananchi wa kijiji cha Mnamila wilayani Buhigwe.
Kikundi cha wanakwaya kikiwa tayari kwa kutumbuiza katika mkutano wa Dk John Pombe Magufuli katika kijiji cha Mnamila.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akifurahia na mgombea ubunge wa jimbo la Buhigwe Mh Obama.
Ilikuwa ni furaha kwa watoto hawa kumuona Dk John Pombe Magufuli.
Watu waliowengi walijipamba
picha za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli kila alipokuwa akipita na
kuzungumza nao katika jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269