Baada ya
kuanza kwa vipigo vitatu mfululizo katika ligi kuu soka nchini Afrika
Kusini, klabu ya soka ya Free States Stars FC anayoichezea mtanzania
Mrisho Ngassa sasa imeibuka katika mechi yake ya nne na kupata ushindi
mnono.
Free
States Stars Fc ikicheza kwa uhakika zaidi katika uwanja wake wa
nyumbani, imewalaza Chipa United kwa jumla ya magoli 3-0 na kukusanya
points tatu muhimu kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu.
Ushindi
huo umekuja mara baada ya klabu ya Free States Stars kumfungisha virago
aliyekua kocha wao na kumpa mkataba kocha mpya ambaye ameleta mabadiliko
makubwa kiuchezaji kikosini.
Mtanzania
Mrisho Ngassa ameendelea kutesa tu kutokana na kuendelea kuaminiwa na
hata mwalimu mpya kwa kucheza katika dakika zote tisini akicheza nafasi
ya kiungo mshambuliaji.
Magoli
haya matatu yalifungwa na mshambuliaji raia wa Ubelgiji mara mbili Andre
Filecia huku lingine likifungwa na mzawa Danny Venter.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269