.

6 WAKAMATWA KWA KUUZA MTOTO NIGERIA

Oct 31, 2015


Wanasema uchungu wa mwana aujua ni mzazi.
Mama mzazi.
Lakini nchini Nigeria uchungu wa mtoto mmoja wa wiki mbili aujua ni mama bandia aliyekuwa na dola mia tisa pekee.
Amini usiamini mama mzazi wa mtoto ambaye hata damu ya uzazi haijaisha amewashangaza watu baada ya kumuuza mwanaye ili angalau apate senti.
Hayo yalibainika baada ya Polisi nchini Nigeria kuwakamata watu sita katika eneo la Kusini Mashariki mwa Nigeria wakituhumiwa kwa makosa ya kumuuza mtoto mchanga wa wiki mbili .
Polisi katika jimbo la Cross River wanasema kuwa miongoni mwa wale waliotiwa mbaroni ni pamoja na mamake mtoto huyo.
Licha ya kuwa hata uchungu wa uzazi alikuwa bado anao, mama huyo mzazi alisema kuwa umasikini mkubwa ndio uliomlazimisha kumuuza mwanawe kwa karibu dola mia tisa pekee yake.
Ulimwengu umepasuka wapi ?
Jimbo hilo limekua na matukio ya muda mrefu ya kile kinachoitwa ''viwanda vya watoto'.
Viwanda vya watoto ni hali ambapo wanawake wanahamasishwa ama kulazimishwa kupata mimba na kisha kuwauza watoto wao wachanga kwa nia ya kupata faida haswa kutoka kwa watu wenye pesa lakini hawana uwezo wa kupata watoto wao wenyewe.
Mnamo mwaka 2013, matineja wasichana 17 waliokuwa wajawazito na watoto wachanga 11 waliokolewa kutoka kwenye nyumba moja jimbo la IMO kusini mashariki mwa nchi hiyo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช