.

WAFUNGWA 6,000 WACHIWA HURU MAREKANI

Oct 31, 2015


Wafungwa 6,000 wameachiwa huru nchini Marekani katika jitihada za kupunguza msongamano katika magereza.
Kwa mujibu wa idara ya haki ya Marekani mpango huu unawalenga wafungwa waliopatikana na makosa ya kumiliki , kuuza na ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Hii ndio mara ya kwanza kwa idadi kubwa kama hii ya wafungwa kuachiwa huru nchini humo.
Idara ya haki inawalenga wafungwa ambao hawana historia ya kutumia nguvu ambao idadi yao inakisiwa kuwa ni nusu ya wafungwa wote nchini Marekani.
Takriban thuluthi moja ya watu wanaotarajiwa kuachiwa huru ni wageni na hao inatarajiwa kuwa watarejeshwa makwao.
Asilimia kubwa ya wafungwa hao waliachiwa huru ijumaa.
Kundi la pili la wafungwa litaruhusiwa kuondoka jumanne ijayo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช