.

DIAMOND ATWAA TUZO YA MTV EMA NCHINI ITALIA

Oct 26, 2015

dimaond
 Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na tuzo yake kutoka MTV EMA.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ jana ametwaa tuzo ya MTV EMA katika kipengele cha ‘Best Worldwide Act: Africa/India’ akimgalagaza Miss World 2000, Priyanka Chopra. Diamond alikuwa akichuana na muigizaji wa filamu na aliyekuwa Mrembo wa Dunia (Miss World 2000), Priyanka Chopra katika tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) kwenye kipengele hicho. 
Priyanka-Chopra-2
Miss World 2000, Priyanka Chopra.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond amewashukuru sana mashabiki wake, wasanii wenzake, uongozi wake pamoja na familia yake huku akisema kutokana na zoezi la uchaguzi mkuu hapatakuwepo na mapokezi makubwa ila itaandaliwa siku maalum kwa ajili ya kupiga picha na tuzo hiyo. Hivi ndivyo Diamond alivyoandika:
 diamond 
Tuzo hizo zilitolewa jana Oktoba 25, 2015 jijini Milan, Italia.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช