.

MAMBO YATAKAYOSABABISHA KURA YAKO IWE IMEHARIBIKA AU SAHIHI

Oct 24, 2015

Kura halali zitakazopigwa siku ya Jumapili kwa ajili ya kuwachagua viongozi kwenye Uchaguzi Mkuu zinaweza kuharibika ikiwa hazitapigwa kwa usahihi na kuondoa utata..
Kura iliyoharibika ni ile ambayo:
  1. Haina alama yoyote
  2. Imepigwa kwa wagombea zaidi ya mmoja
  3. Imeandikwa jina la mpiga kura
  4. Alama imewekwa nje ya kisanduku cha picha ya mgombea
  5. Haina muhuri wenye alama rasmi
Kura sahihi;
  1. Yenye alama ya ‘v’ kwenye kisanduku
  2. Yenye alama yoyote kwenye kisanduku/picha/ jina la mgombea
Utata
Kutakuwa na utata endapo utaweka alama iliyopitiliza kisanduku cha mgombea mmoja na kufika kwa mwingine. Epuka kuharibu kura. Kura yako, mustakabali wako

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช