Breaking News

Your Ad Spot

Oct 24, 2015

MTOTO HATUMWI DUKANI LEO . NI KATIKA UFUNGAJI WA KAMPENI ZA CCM JIJINI MWANZA

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Pichani) amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya shughuli ya kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu kitaifa kwa upande wa Chama hicho inayotarajiwa kufanyika hii leo katika Uwanja wa CCM Kirumba yamekamilika.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Screen kubwa itafungwa nje ya uwanja huo kwa ajili ya wale watakaokosa nafasi ya kuingia uwanjani kwa kuwa shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na Maeneo jirani.
Mbali na Mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli kuwepo katika mkutano huo, pia Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaemaliza muda wake Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi watakaohudhuria katika Mkutano huo wa Ufungaji wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa upande wa CCM 
Wakati Watanzania wakitarajia kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu siku ya kesho jumapili ya Octoba 25, Chama cha Mapinduzi CCM kimejihakikishia ushindi mnono katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia ngazi ya udiwani, Ubunge na Urais.
Shamra shamra kwa makada wa CCM zimepamba moto katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza katika kuelekea kwenye ufungaji wa kampeni za chama hicho kitaifa unaofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages