.

MKUTANO WA HADHARA WA UFUNGAJI WA KAMPENI ZA CCM PEMBA

Oct 23, 2015

x1
Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maelfu ya wanachama cha Mapinduzi CCM na wananchi wa Kisiwani Pemba wakati alipokuwa akiomba kura pamoja na kuwaombea wagombea wengine wa CCM akiwemo Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama hicho uliofanyika leo katika uwanja wa Gombani yakale.
x2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na Maelfu ya wanachama cha Mapinduzi CCM na wananchi wa Kisiwani Pemba katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama hicho katika uwanja wa Gombani yakale leo na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM.
x3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia maelfu ya wanachama cha Mapinduzi CCM na wananchi wa Kisiwani Pemba katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama hicho katika uwanja wa Gombani yakale leo pamoja na kuwaomba kura wananchi pia na kuwaombea Kura wagombea wa Chama hicho.
[Picha na Ikulu.]

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช