Breaking News

Your Ad Spot

Oct 28, 2015

SABABU 8 ZA KUFUTWA KWA UCHAGUZI ZANZIBAR

Hizi ndizo sababu nane zilizotolewa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa kisiwani Zanzibar Bw Jecha Salim Jecha kuhusu kufutiliwa mbali kwa matokeo ya uchaguzi wa eneo hilo.
1. Makamishna wa uchaguzi katika tume hiyo walipigana kutokana na tofauti zao
2. Makamishna walikuwa na upendeleo fulani.
3. Katika vituo vyengine, hususan kisiwani Pemba, ambacho ni miliki ya Zanzibar, kura zilizopigwa zilikuwa zaidi ya zilizosajiliwa.
4. Masanduku ya kupigia kura hayakupewa ulinzi wa kutosha na maajenti pamoja na maafisa wa uchaguzi.
5. Maajenti wa vyama walifukuzwa katika vituo kadhaa.
6. Vijana walivamia vituo vya kupigia kura wakiwa na lengo la kuzua ghasia.
7. Vyama vya kisiasa vimekuwa vikiingilia tume hiyo.
8.Kura ziliharibiwa hususan zile kutoka Pemba.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages