Breaking News

Your Ad Spot

Nov 30, 2015

DAKTARI RUKSA KUNYWA POMBE KWA KIBALI


Watu 60,000 wapewa idhini ya daktari kunywa pombe India

Licha ya jimbo la Gujarat India kupiga marufuku unywaji utengenezaji na unywaji pombe, takriban watu 60,000 wamepewa idhini ya kunywa tembo.

Takwimu zilizowekwa wazi na idara ya afya inaonesha kuwa watu 60,000 wamepewa idhini na madaktari kunywa pombe
katika jimbo hilo ambapo adhabu ya ni kali.

Haijulikani ni ugonjwa upi huo unaotibika na pombe ila inaaminika watu hujilinda kwa idhini hizo za daktari kuepuka hatari ya kushikwa .
Ukipatikana ukinywa pombe bila idhini unatozwa faini ya dola 20.

Gujarat, ndiko alikozaliwa kiongozi wa kwanza wa taifa Mahatma Gandhi.
Jimbo hilo liliharamisha ulevi mwaka wa 1960 kwa heshima wa kiongozi huyo wa taifa.


Ukipatikana ukinywa bila idhini unatozwa faini ya dola 20

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages