Breaking News

Your Ad Spot

Nov 30, 2015

ATHARI ZA JOTO DUNIANI KUJADILIWA

Wanaharakati wakiandamana Ujerumani kutaka hatua
zichukuliwe kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Mazungumzo kuhusu Mabadiliko ya tabia nchi yanaanza rasmi
asubuhi ya leo huko jijini Paris nchini ufaransa, wakuu wa nchi zaidi ya mia na
hamsini wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo uliondaliwa na umoja wa mataifa.

Maandamano yamefanayika duniani kote kushinikiza
kuchukuliwa hatua kupambana na ongezeko la joto duniani, jijini Paris Polisi
walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji huku
watu mia moja wakishikiliwa kwa kosa la kukiuka amri ya kutofanya maandamano
iliyotolewa baada ya mashambulizi jijini humo.

Akifungua mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa
Laurent Fabius, alisema ana uhakika kuwa mazungumzo hayo yatawafikisha kwenye
hatua ya makubaliano chanya.



Wakati huo huo rais Obama amezuru kituo cha burudani cha
Bataclan mjini Paris kutoa heshima zake kwa waathiriwa na shambulio la kigaidi
wiki mbili zilizopita. Obama na rais wa nchi hiyo, Francois Hollande waliweka
shada la maua kwenye ukumbi huo, ambako watu tisini waliuawa na wanamgambo wa
Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages