Vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mbunge Angelina Malembeka,kwa kata 18 katika Mkoa wa Kaskazin Unguja.
Baadhi ya viongozi wa Wadi(kata) wakimsikiliza Mbunge Angelina Malembeka katika kikao kilichofanyika katika Afisi za CCMJimbo la Kitope,Kaskazin unguja
Malembeka akiwa katika meza kuu tayari kugawa vifaa vya michezo kwa viongozi wa kata.
Wito umetolewa kwa vijana kupenda michezo kwani michezo ni afya,furaha,amani na upendo na kwa kupenda michezo kutawafanya vijana kuaacha kukaa vijuweni
Wito huo umetolewa na mbunge wa viti maalum kupitia CCM wa Mkoa wa Kaskazin Unguja,Bi Angelina Malembeka,katika mkutano wake na vijana wa uvvcm wa mkoa huo.
Bi malembeka ,ametoa vifaa vya michezo kwa vijana hao ili kuwawezesha kuanzisha ligi itakayo shirikisha timu za kata ili kumpata mshindi katika mashindano hayo.
Vifaa vilivyotolewa ni jezi 18 na mipara miwili kwa kila timu na kuwataka vijana hao kuunda timu kila kata na kuanzisha mashindano ya kata ili kukuza vipaji na kuibua vipaji vipya.
Vkizungumzia zawadi katika mashindano hayo,amesema mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi million moja,mshindi wa pili sh lakitano,mshindi wa tatu laki tatu na mshindi wanne shilingi laki moja na nusu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269