Kipindi hiki ni moja ya vipindi adimu katika Radio, ambacho hurushwa na Mtangazaji Mbazigwa Hassan (Pichani) akishirikiana na mkongwe wa muziki nchini mwenye asili ya Congo-DRC, Tshimanga Kalala Assossa 'Papaa Tshim'.
Akizungumza na Chachandu Daily leo, mtayarishaji wa kipindi hicho kaka Mbazigwa, au Mzee wa Kavasha, amesema, Jumamosi hii, anatarajia kuwa na mamabo mazito wakati wa kipindi hicho kitakachoanza saa 11 aflajiri hadi saa 3.00 asubuhi.
Katika kipindi hicho wasikilizaji watapa fursa ya kutafsiriwa moja ya nyimbo za Kilingala, ambapo Jumamosi hii, itaendelea tafsiri ya wimbo 'Antention na Sida' wa TP Ok Jazz ulioimbwa na bendi hiyo chini ya Marehemu Franco Lwambo Lwanzo Makiadi. Pia mtangazaji atakuletea mazungumzo na wanamuziki mbalimbali wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wapo ndani ya nchi hiyo na nje kama Paris, Ivory Coast, Uingereza na kwamba wanamuziki maarufu waliopo nje ni kama Profesor Vatta Mombasa 'Jujumen' ambaye yupo nchini Ivory Coast na Nzaya Nzayadyo aliyepo Uingereza na na Nyboma Mwandido ambao w aliwahi kupigia Lipua Lipua katika miaka ya 70, ambapo viliporomoshwa vibao kama 'Kinzengenzenge' na 'Andoya'.
Ili kuwa karibu na kupata uhondo huu, fungua 94.6 TBC FM kwa wale wa Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar
Your Ad Spot
Jan 5, 2011
Home
Unlabelled
ASSOSA NA MBAZIGWA HASSAN KUUNGURUMA JUMAMOSI HII KATIKA KIPINDI CHA' KAVASHA TIME'
ASSOSA NA MBAZIGWA HASSAN KUUNGURUMA JUMAMOSI HII KATIKA KIPINDI CHA' KAVASHA TIME'
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
mkuu twashukuru sana kutupa taarifa hiz. tutakuwepo Insha-Allah
ReplyDelete