Breaking News

Your Ad Spot

Nov 4, 2015

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUJIUNGA NA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU

oh1 
Mahmoud Ahmad Arusha
Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu amezitaka nchi za Afrika kujiunga na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu ilikutekeleza matakwa ya wananchi kupata haki yao ya kupata masuala ya kisheria kwa upana Zaidi na kuweka msukumo katika suala hilo.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiongea na waandishi wa habari aliposhiriki kongamano la pili linalojadili Masuala ya upatikanaji wa haki za binadamu na kuandaliwa na mahakama ya Afrika ya haki za binadamu yenye makao makuu jijini Arusha.
Jaji Makungu alisema kuwa mkutano huo ni sehemu ya kupata uzoefu na kujua wenzao kote duniani wanavyoshiriki katika kutoa haki kwa Raia pindi wanapopeleka masuala yao Mahakamani na itasaidia kuendesha mashauri ya kesi mahakamani kwa haraka Zaidi na kutoa hukumu kwa muda muaafaka bila manung’uniko.
Alisema kuwa ifike mahali Tanzania ikajiunga na kufuata sharia na hukumu za mahakama hiyo kwani zitaweka wigo mpana wa Raia kupata haki zao kusikilizwa kwa upana katika mahakama za hapa nchini na pia katika mahakama ya Afrika ya haki za binadamu pindi wanapoona kuwa hawakutendewa haki na mahakama za hapa nchini.
“Nazishauri nchi ambazo bado hazijajiunga zifanye hivyo ilikuweka usawa wa wananchi kupata haki zao pindi wanapoona mahakama za chini hazijawatendea haki na hivyo kuwapasa kupeleka mashauri yao katika mahakama za juu Zaidi ikiwemo mahakama hiyo ya Afrika ya haki za binadamu”alisema Jaji Makungu
Alisema kuwa kuna baadhi ya kesi za hapa nchini zimefunguliwa na wananchi ikiwemo ya marehemu mchungaji Mtikila ambayo hadi mda huu hukumu haijatekelezwa kutokana na katiba kutokamilika hivyo akaishauri serikali kuifanyiakazi suala hilo ilikuendana na mikataba iliyojiunga.
Mkutano huo wa pili wa masuala ya haki za binadamu utakaofanyika kwa siku tatu utasaida kukuza uelewa wa uendeshaji kesi na wananchi kupata fursa za kupeleka mashauri yao wanayoona kuwa hawajatendewa haki na mahakama za nchi husika katika bara la Afrika.
Hadi sasa ni nchi 29 tu katika ya nchi 54 ndio zimejiunga na mahakama hiyo zikitekeleza maagizo ya umoja wa Afrika na nchi 7 ndio zimeridhia wananchi wao kupeleka mashauri mahakama hiyo.
Nchi hizo ni Tanzania,Mali,Burkinafaso,Ivory Coast,Rwanda,na Malawi ambazo zimeridhia wananchi wao kupeleka mashauri yao kwenye mahakama ya Afrika ya haki za binadamu ambapo hadi sasa bado hazijatekeleza huku zilizotolewa na mahakama hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages