Breaking News

Your Ad Spot

Dec 30, 2015

LEICESTER CITY WAMEIDHIBITI MAN CITY NDANI YA DIMBA LA KING POWER

Ligi Kuu soka Uingereza imeendelea tena usiku wa December 29 kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la King Power, mchezo wa December 29 ulikuwa unazihusisha klabu za Leicester City dhidi ya klabu ya Manchester City. Uzuri wa mchezo huu ni kuwa vilabu vyote viwili vipo katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu kutokana na nafasi walizopo katika msimamo wa Ligi.
1636
Man City walikuwa ugenini kuwakabili wenyeji wao Leicester City, klabu ambayo inafanya vizuri na kuwatishia timu vigogo vya Ligi Kuu Uingereza, klabu ya Leicester City ambayo safu yake ya ushambuliaji ilikuwa inaongozwa na Jamie Vardy na mchezaji wa kimataifa wa Algeria Riyad Mahrez ilishindwa kutamba katika dimba lake la King Power.
927
Licha ya kila timu kuonesha jitihada za kutaka kupata walau goli moja litakaloiwezesha kuvuna point tatu muihimu, mchezo ulikuwa mgumu na hatimae, dakika 90 zilimalizika kwa sare ya kutofunga. Pamoja na Man City kuwa na nyota wake kadhaa kama Yaya Toure na Sergio Aguero walishindwa kupenya ngome ya Leicetser City iliyokuwa inaongozwa na  Kasper SchmeichelWes Morgan na Robert Huth.
4151

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages