Breaking News

Your Ad Spot

Dec 25, 2015

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA SHEREHE ZA MAULID ZANZIBAR

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Msaidizi Mkoa wa Magharibi  Zanzibar Suleiman Mzee (CHARAS) alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar Dec 24, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria  Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,   akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu  Mohammed Gharib Bilal, alipowasili nyumbani kwake Migombani Zanzibar  Dec 24, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yanayofanyika kila mwaka.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mohammed Gharib Bilal katikati, akiwatambulisha wake zake kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kushoto alipowasili nyumbani kwake Migombani Zanzibar Dec 24, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria  Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yanayofanyika kila mwaka. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages