Breaking News

Your Ad Spot

Dec 30, 2015

USHINDI WA AZAM FC WAISHUSHA YANGA KILELENI, CHEEEE

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo December 30 kwa mchezo mmoja wa kiporo kumaliziwa katika dimba la Azam Complex Mbande Chamazi. Huu ni mchezo ambao ulikuwa unakutanisha timu ambazo zinatafuta nafasi ya kusogelea kuelekea kileleni mwa msimamo wa Ligi.
DSC_0192
John Bocco akijaribu kumkabili beki wa Mtibwa Sugar Salim Mbonde
Mchezo wa December 30 ulikuwa unazikutanisha timu ya Azam FC dhidi ya klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani. Huu ni mchezo uliokuwa umeteka hisia za watu wengi, kwani matokeo ya ushindi kwa Azam FC yalikuwa yanaishusha Yanga kileleni.
DSC_0208
Andrew Vicent akijaribu kumdhibiti Farid Musa wa Azam FC
Katika dimba la Azam Complex licha ya klabu ya Mtibwa Sugar kuwa ugenini walifanikiwa kumiliki mpira kwa muda mwingi, lakini Azam FC walionekana kutulia na kucheza kwa mbinu kwa kiasi kikubwa. Mtibwa Sugar ambao nahodha wao Shabani Nditi aliingia akitokea becnhi baada ya kupona majeruhi. Walikubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Azam FC.
DSC_0227
Ramadhani Singano ‘Messi’ baada ya kumtoka beki wa Mtibwa Sugar
Mtibwa Sugar walifanya makosa dakika ya 88 baada ya kumfanyia faulo nahodha wa Azam FC John Bocco nje kidogo ya eneo la hatari, hivyo Azam FC kupitia John Bocco wakapiga faulo hiyo na kupachika goli la ushindi na kufanya mechi kumalizika kwa Azam FC kuibuka ushindi  wa goli 1-0.
DSC_0220
Kipre Tchetche baada ya kumpiga chenga Andrew Vicent
Kwa matokeo hayo Azam FC wanakuwa wanaongoza Ligi na kuishusha Yanga ambao walikuwa wamekaa kileleni kwa kuizidi michezo Azam FC. Yanga sasa wana jumla ya point 33 wakiwa wamecheza michezo 13, wakati Azam FC wana jumla ya point 35 wakiwa wamecheza michezo sawa na Yanga.
DSC_0235
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli la John Bocco
DSC_0247
Mashabiki wa Azam FC wakishangilia ushindi wa timu yao

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages