Breaking News

Your Ad Spot

Dec 23, 2015

WAZIRI KITWANGA ATANGAZA OPERESHENI KALI YA KUWASAKA WAHAMIAJI HARAMU POPOTE PALE WALIPO NCHINI



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, 2015. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Katika hotuba yake, licha ya maelekezo mengine aliyoyatoa kwa viongozi wakuu, pia aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanza rasmi kwa operesheni ya kuwasaka na kuwakamata wahamiaji haramu popote walipo nchini na kuagiza msako huo kuanza mara moja Januari 1, 2016. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji

Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za  Kusafiria,  Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo, na wapili kulia (waliokaa) ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile na kulia ni Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha),  Piniel Mgonja
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wasita kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.  Wasita kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile




Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanz rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages