Breaking News

Your Ad Spot

Dec 30, 2015

WAZIRI MKUU AFUNGWA JELA, NI BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA KULA RUSHWA

 WAZIRI Mkuu wa zamani wa Israeli, Bw. Ehud Olmert, akiwa mahakami mjini Jerusalem


Na K-Vis Media na Mashirika ya Habari
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Israeli, Bw. Ehud Olmert, ametupwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kula “mlungula” RUSHWA.
Olmert ambaye amerithiwa na Waziri Mkuu wa sasa Benjamin Netanyahu, alihukumiwa kifungo cha miaka 6 jela na mahakama ya chini mnamo mwaka 2014, lakini adhabu hiyo ilipunguzwa na mahakama kuu hadi kufikia kifungo cha miezi 18 jela leo Jumatatu Desemba 28, 2015.
Olmert mwenye umri wa miaka 70, aliendesha operesheni ya kuwashambulia Hezbollah huko Lebanon, wakati wa utawala wake na kusababisha vifo vingi, alihukumiwa kufuatia mikataba ya majumba ya kupangisha wakati huo akiwa Meya wa mji wa Jerusalem kabla ya kuwa waziri Mkuu mnamo mwaka 2006.
Olmert ambaye aliondoka madarakani mnamo mwaka 2009, anakuwa Kiongozi wa juu wa kwanza wa Israeli kutupwa jela na anatarajiwa kuanza kutumikia kifungo chake mnamo Februari 15 mwaka ujao 2016

 Akijadiliana jambo na wakili wake
 Akiwa mahakamani
 Wakati huo akiwa madarakani
Akiwasili mahakamani huku akisindikizwa na walinzi wake

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages