.

MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA AKUTANA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI DAR ES SALAAM

Sep 30, 2015

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC)  Jaji Mstaafu  Damian Lubuva akizungumza jambo na wamiliki wa vyombo mbalimbali vya Habari (pichani hawapo) walipokutana   Dar es Salaam leo Sarena,  kuzungumzia maswala ya uchaguzi wakati wa Mkutano wa Tume hiyo na Wamiliki wa vyombo vya habari uliofanyika katika Hoteli ya Sarena Jijini Dar es Salaam leo.
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Emanuel Kawishe
 Wawakilishi  wa nyombo vya habar
 Wanahabari wakiwa kazini wakati wa Mkutano wa Tume ya Uchaguzi walipokutana  na Wamiliki wa vyombo vya habari uliofanyika katika Hoteli ya Sarena Jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC) aliyekaa Jaji Mstaafu  Damian Lubuva akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) Rgnald Mengi wakati wa Mkutano wa Tume hiyo na Wamiliki wa vyombo vya habari uliofanyika katika Hoteli ya Sarena Jijini Dar es Salaam .

DK.SHEIN AENDELEA NA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI KATIKA VIWANJA VYA GARAGARA MTONI ZANZIBAR

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni Zanzibar kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua tena kuongoza Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndg Yussuf Mohammed akizungumza na Wananchi na WanaCCM katika viwanja vya garagara mtoni wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na kuwatana Wananchi kumpigia kura Dk Shein, ili kuzidi kuleta maendeleo katika Visiwa vya Unguja na Pemba katika kipindi cha miaka mitano ijayo. 
Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya garagara wakihudhuria mkutano wa kampeni ya mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, (P.T)
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urai kupitia CCM katika viwanja vya garagara Mtoni Zanzibar. 
Mama Fatma Karume akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viiwanja vya Garagara mtoni Zanzibar na kuwataka siku ikifika kutia kura ya Ndio kwa Dk Ali Mohamed Shein, 
Wananchi wakimshangilia Mama Fatma Karume wakati akiwahutubia katika mkutano wa Kempeni ya Mgombea ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Wasaani wa Bendi ya Moto wakitowa burudani kuhamasisha  Wanachama wa CCM wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, zilizofanyika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mambo ya Yomoto Bendi hayo katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika viwanja vya garagara wakimuombea Kura Dk Shein, wakati wa kampeni yake.  
Wanachama wa CCM wakifuatilia burudani hiyo wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika viwanja vya garagara mtoni akiwa katika mikutano yake ya kampeni ya kugombea Urais wa Zanzibar. kwa kupata ridhaa za Wananchi kuongoza Zanzibar kwa Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar katika sekta mbalimbali na kudumisha Amani na Utulivu katika Visiwa vya Unguja na Pemba. 
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa Mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar na kutowa sera za CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ya kipindi chake baada ya kupata ridhaa za Wananchi kumpa kura ya Ndio.katika uchaguzi mkuu mwa huu.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akifuatilia Sera za CCM wakati Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa mkutano wake wa kampeni katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar
Wanachama wa CCM wakifuatilia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya garagara mtoni 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Welezo Zanzibar kupitia CCM Saada Mkuya katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtoni Zanzibar wakati wa mkutano wa kampeni za Urais wa Zanzibar Dk Shein katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mfenesini Zanzibar Kanali Mstaaf Khamis , wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Uwakilishi wakati wa mkutano wa kampeni za Urais zilizofanyika katika viwanja vya garagara Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mfenesini Zanzibar Mhe Machano Othman akizungumza kwa niaba ya wagombea wezake katika mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea wa Udiwani wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM uliofanyika katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akiagana na Viongozi wa CCM baada ya kumalizika kwa mkutano wa Kampeni katika viwanja vya garagara mtoni Zanzibar 
Imetayarisha na (Othman Mapara).Blogspot. Zanzinews.com.

MAZISHI YA WAZIRI KOMBANI MKOANI MOROGORO

 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiweka udongo katika kaburi la marehemu Kombani.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiweka udongo katika kaburi la marehemu Celina Kombani. Nyuma yake ni Samia Suluhu.
Mama Salma Kikwete naye akiweka udongo kwenye kaburi la Kombani.
Bwana Hemed Saleh Pongoleni ambaye ni mume wa marehemu akiweka shada la maua katika kaburi la mke wake, Celina Kombani.
Watoto wa marehemu wakiwa na mashada ya maua wakati wa maziko ya mama yao.
Viongozi mbalimbali wakishiriki maziko hayo.Jeneza lenye mwili wa marehemu Celina Kombani likiingizwa kaburini.
Jeneza likiombewa kabla ya kuingizwa kaburini.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho mbele ya mwili wa Waziri Celina Kombani katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akiaga mwili wa Waziri Kombani leo.
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda akitoa heshima zake mbele ya jeneza lenye mwili wa Waziri Celina Kombani kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

AJALI YA BASI LA NGORIKA YAUA ASKARI WA JWTZ NA KUJERUHI WENGINE 33


Watu wawili wamefariki dunia akiwemo askari wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na wengine 33 kujeruhiwa baada ya basi mali ya kampuni ya Ngorika kuigonga kwa mbele Toyota Costa eneo la Misugusugu mjini Kibaha .

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 1.30 asubuhi jana wakati basi hilo likitokea Dar esalaam kwenda Arusha ambapo ilipofika eneo hilo dereva alihama upande wake wa njia kuyapita magari mengine yaliyokua mbele yake bila tahadhali hivyo kwenda kugongana uso kwa uso na costa iliyokua ikitokea Miono Bagamoyo kwenda Dar esalaam.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jafari Mohamed amethibitisha tukio hilo na kutaja waliokufa ni Rutta Saimon mwalimu wa shule ya msingi Mwambao Bagamoyo na Peter Maro askari wa JWTZ na kwamba anasadikiwa kuwa ni wa Kikosi cha Jeshi la Nyumbu Kibaha na wote walikua abiria katika Costa hiyo.

Kamanda Jafari amesema kati ya majeruhi hao 33, wanne hali zao ni mbaya kutokana na kuvunjika sehemu mbalimbali za mwili.

"Majeruhi wote wa ajali hiyo walipelekwa Tumbi na walitibiwa na wengi wao wameruhusiwa kuendelea na safari yao lakini hao wanne ndiyo wamelazimika kulazwa hapo kwa matibabu zaidi kutokana na hali zao kuwa mbaya maana wamevunjika sehemu mbalimbali za mwili, na pia miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini humo kusubiri ndugu "amesema Kamanda Jafari.

MAGAZETI YA LEO SEPT 30, 2015


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
ยช