Breaking News

Your Ad Spot

Jan 27, 2016

BOMOA BOMOA YAENDELEA KUPINGWA MAHAKAMANI DAR

 Lile zoezi la kubomoa nyumba zinazodaiwa kujengwa maeneo "hatarishi", mabondeni limeendelea kupingwa leo Januari 27, 2016, ambapo wakazi wa jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na diwani wao, Patrick Asenga (pichani juu), wametinga mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha ardhi pale katikati ya jijini mtaa wa Samora, wakipinga kusudio la kuvunjiwa nyumba zao zipatazo 2651. Pichani diwani huyo akizunhumza na waandishi wa habari juu ya hatua wanazochukua sasa. K-VIS MEDIA ilishuhudia mamia ya wakazi hao wengi wao wakiwa wanawake, wameketi pembezoni mwa barabara ya Samora, wakisubiri shauri hilo. (Picha; K-VIS MEDIA)








No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages