Mkurugenzi asiye mtendaji wa
kampuni ya ndege ya Fastjet Balozi Ami Mpungwe, akizungumza na wasafiri
wakati wa kuanzisha safari za ndege hiyo kwenda Nairobi kutokea uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es
Salaam, kutoka kulia ni mkurugenzi asiye mtendaji Lawrence Masha, Meneja
mkuu wa kampuni hiyo (Afrika Mashariki) Jimmy Kibati na Meneja wa
mahusiano kati ya Fastjet na Serikali, Mhandisi August Kowero.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya,
John Haule (kulia) akikata utepe ili kuikaribisha ndege ya Fastjet
nchini Jijini Nairobi mara baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta jana, kushoto kwake ni Meneja mkuu wa Fastjet
Afrika Mashariki Jimmy Kibati na Mkurugenzi asiye mtendaji balozi Ami
Mpungwe.
Wageni mashuhuri wakishirikiana
na viongozi wa Fastjet kukata keki mara baada ya ndege kuwasili katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi jana,
kutoka kushoto ni Meneja mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki Jimmy Kibati,
mkurugenzi asiye mtendaji Ami Mpungwe, Balozi wa Tanzania nchini Kenya
John Haule, Mkurugenzi asiye mtendaji Lawrence Masha na Meneja Masoko na
Maendeleo ya Biashara wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini Kenya
(KAA) William Simbah.
Ndege ya Shirika la Ndege la
fastjet ilikiwasili kwenye uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwa
mara ya kwanza baada ya kuanza safari zake kati ya Dar es Salaam na
Nairobi nchini Kenya
Meneja mkuu wa kampuni hiyo
(Afrika Mashariki) Jimmy Kibati juu pamoja na wafanyakazi wa Ndege hiyo
wakishuka kwenye ndege mara baada ya kutua kwenye uwanja wa Ndege wa
Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya,
John Haule (kulia) akiwa katikapicha ya pamoja na Meneja mkuu wa Fastjet
Afrika Mashariki Jimmy Kibati na Mkurugenzi asiye mtendaji balozi Ami
Mpungwe mara baada ya kuikaribisha ndege ya Fastjet nchini Jijini
Nairobi wakati ndege hiyo kutua katika uwanja wa kimataifa wa Jomo
Kenyatta jana, kwa mara ya kwanza.
……………………………………………………………………………………………………..
Kampuni ya ndege ya Kiafrika
yenye gharama nafuu fastjet,imepanua mtandao wake wa safari barani
Afrika kwa kuwa na safari za kimataifa za kila siku kutoka Dar es
Salaam na Kilimanjaro kwenda Nairobi na hali kadhalika safari za ndani
za kila siku kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar.
Uzinduzi wa safari za anga za
fastjet kutoka Dar es Salaam hadi Nairobi, Kilimanjaro hadi Nairobi na
Dar e s Salaam kwenda Zanzibar zote zimefanyika Januari 11, 2016 na
hivyo kufanya iwe ni hatua muhimu katika kujipanua katika safari zake
kimataifa na kitaifa.
Safari za kila siku kwenda
Zanzibar zinatarajiwa kuwarahisishia watanzania walio wengi pamoja na
wageni wa kimataifa kuitembelea Zanzibar,kukuza utalii na biashara
pamoja na kuchangia kwa kiwango kikubwa kwenye kukua kwa uchumi visiwani
humo.
Kuzinduliwa kwa safari za
fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es Salaam kunaanzisha enzi mpya ya
abiria ambao wamekuwa wakitaabika kwa tozo kubwa ya nauli kwa usafiri wa
anga kati ya nchi mbili za Afrika Mashariki ambazo uchumi wake unakua
kwa kasi.
Matokeo ya safari za fastjet
nchini Kenya tayari yameshaanza kujadiliwa, yakikolezwa na ukweli kwamba
nauli dhidi ya mashirika washindani yanayofanya safari kati ya nchi
hizi mbili ambako ni kushuka kwa kasi hadi ya asilimia 40 siku ya
kwanza tu tangu fastjet
ilipotangaza kuanzishwakwa safari zake kati ya Kenya na Tanzania.
Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania
John Corse anasema, “ukweli ni kwamba ushindani ni mzuri kwa abiria.
Unaleta nafasi kuchagua jinsi ya kusafiri na pia unasababisha nauli
kushuka.”
Nauli za fastjet kimsingi ziko
chini kuliko nauli zinazotozwa na mashirika mengineya ndege ambayo
hivi sasa yanafanya safari kati ya Tanzania na Kenya ambapo nauli za
fastjet kutoka
Kilimanjaro/Nairobi ni kuanzia dola 50 kw safari moja na ya kwenda Dar es Salaam/Nairobi
ni dola 80 kwa safari moja. Nauli hizo hazijumuishi kodi za serikali ambazo ni dola
49kwa kuondokea Tanzania na dola 40 kwa kuondokea Kenya na hivyo fastjet
kuwashauri abiria kukata tiketi zao mapema ili kuitumia fursa hiyo ya nauli ya bei
nafuu. fastjet inatarajia kuongeza safari moja zaidi kwenye niia yake mpya ya Kenya
kutokan ana mahitaji ya wateja
kuongezeka kutokana na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati na
tayari imeshaonesha kwamba inatarajia kuzindua safari kati ya
Zanzibar na Nairobi na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka huu 2016.
“Kama ambavyo imekuwa kwa njia
zetu nyingine ambazo fastjen timezindua tunatarajia abiria wetu walio
wengi kwenye njia yetu mpya Kenya kuwa abiria wa kwanza ambao huenda
wasingemudu kusafiri kwa njia ya anga hapo awali,” anabainisha Corse.
Matarajio haya yanaungwa mkono na utafiti uliofanywa na fastjet ambao unaonesha
Kuwa zaidi ya theluthi moja ya
abiria watakuwa wanasafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza na hali
kadhalika kumudu usafiri huo kwa mara ya kwanza.
“Usafiri wa anga ambao abiria
wanaumudu ni msingi wa kukua kwa uchumi barani Afrika kutokana na
matokeo chanya yanayosababishwa na bei nafuu ya usafiri wa ndege kwa
maisha ya wananchi na uchumi kwa jumla,”alisema Corse.
“Tunazishukuru wizara za
usafirishaji na mamlaka za usafiri wa anga za Tanzania na Kenya kwa
kufanya kazi pamoja kuwezesha fastjet kutambua dira yetu ya kuongezeka
kwa idadi ya wateja ambao wanaweza kufikia usafiri wa anga wanaoumudu,”
alihitimisha Corse.
Jambo ambalo lina umuhimu zaidi
kwenye njia hii mpya ni njia mbadala ya kuibeba mizigo inayojulikana
kama “freighty” ambayo inaruhusu abiria kusafiri na mzigo hadi kilo 80
kwenye mabegi kwa dola 80. Mbadala huu wa mzigo kimsingi unatarajiwa
kuwa maarufu kwa wafanya biashara wanaosafiri na fastjet kununua bidhaa
za jumla na kuzisafirisha kwa ajili ya kuuzakwenye masoko ya ndani.
Ukataji tiketi unaweza kufanyika kupitia mtandao wa www.fastjet.com,
kupitia wakala waliothibitishwa na fastjet au kwa njia ya mawasiliano
ya simu: +255-784-108900. Malipo ya tiketi yanaweza kufanyika kwa fedha
taslim, kwa njia ya mtandao au kupitia malipo kwa njia ya simu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269