Breaking News

Your Ad Spot

Jan 26, 2016

'MAKTABA YA KUELEA' YATIA NANGA JIJINI DAR ES SALAAM


Meli ambayo imebebea maelfu ya vitabu, ambayo huhudumu kama maktaba, imetia nanga bandarini Dar es Salaam.
Meli hiyo ina zaidi ya vitabu 5,000 pamoja na video.
Itakuwa bandarini Dar es Salaam kwa muda wa wiki tatu hivi, hadi tarehe 17 Februari

Wananchi wataruhusiwa kuingia kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na mbili jioni Jumanne hadi Jumamosi.
Jumapili, itafunguliwa kati ya saa sita unusu mchana hadi saa kumi na mbili jioni. Jumatatu, haitafunguliwa.

Ada ya kiingilio ni Sh1,000 za Tanzania.
Wanaopanga kuingia, wanatakiwa kupepa vitambulisho vya kitaifa au pasipoti.
Nahodha wa meli hiyo ni Bw Durke.
 Wahudumu wote 400 kwenye meli hiyo ni wa kujitolea, hakuna anayelipwa mshahara
 Waziri wa Elimu Tanzania Joyce Ndalichako, aliyelaki meli hiyo bandarini, amesema taifa hilo litapanua huduma za maktaba wilayani na vijijini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages