NA K-VIS MEDIA NA MASHIRIKA YA HABARI
MWANASOKA anayesukuma gozi la kulipwa katika klabuya TP Mazembe ya mjini Lubumbashi nchini CONGO-DRC, Mtanzania Mbwana Ally Samatta, amenyakua tuzo ya mwnasoka bora wa Afriaka anayecheza ligi za ndani ya bara hilo kwa mwaka huu 2015.
Samatta
alinyakua tuzo hiyo usiku wa kuamkia leo
Januari 8, 2015 katika hafla ya kukata na mundu iliyofanyika kwenye kituo cha
mikutano cha kimataifa mjini Abuja nchini Nigeria.
Samatta
amenyakua tuzo hiyo baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 127 mbeleya mchezaji
mwenzake wa TP Mazembe, mlinda mlango mwenye mwembwe nyingi Robert Muteba
Kidiaba ambaye alijikusanyia pointi 88.
Mwanasoka
kutoka Algeria Baghdad Bounedjah alishika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 63.
Samatta
anakuwa mwanasoka wa kwanza kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kunyakua tuzo
hiyo tangu historia ya mchezo wa kandanda iasisiwe.
Akiwa
na Mazembe Samatta anasifiwa kwa umaridadi wake wa kupachika mabao muhimu na
hivyo kuipatia heshima kubwa timu yake, hali kadhalika amekuwa mchezaji muhimu
anapochezea timuyake ya taifa Taifa Stars.
Historia
ya mwanasoka huyu inaanzia kule Mbagala wilayani Temeke jijiniDar es Salaam
ambako alikuwa akisukuma ndinga na timu kali ya Mbagakla Market na kuiwezesha
kupanda daraja hadi daraja la kwanza na ndipo Simba ilipomuona kipaji chake na
kumchukua.
Hata
hivyo mchezaji huyo mpole, hakudumu muda mrefu Simba kutokana na kiwango
chake na alisajiliwa na klabu hiyo tajiri nchini Congo yaani TP Mazembe
Samatta (wapili kushoto), akikabidhiwa tuzo hiyo.












No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269