Breaking News

Your Ad Spot

Jan 31, 2016

MNADHIMU MKUU MPYA WA JWTZ AAPISHWA IKULU LEO

Amiri Jeshi Mkuu Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016. Awali Luteni Jenerali Mabeyo alikuwa Mkuu wa Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini na anachukua nafasi ya Luteni Jenerali Samwel Ndomba. Rais pia amewaapisha Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala mkoa wa Katavi, huku aliyekuwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Kamishna Clodwin Mtweve kuwa Katibi Tawala mkoa wa Mwanza. Naye Dkt.Mahafhi Juma Maalim aliapishwa kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Kuwait (Habari na K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Picha na Ikulu).
Rais akimpongeza Luteni Jenerali Mabeyo kwa wadhifa huo mpya.
Rais katika picha ya pamoja na Mnadhimu Mkuu mpya wa Jeshi, Luteni Jenerali Mabeyo, na mtangulizi wake, Luteni Jenerali Ndomba.
Rais katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange(wapili kushoto), Mkuu WA Jeshi la Polisi, IGP, Ernest Mangu(watatu kulia), Mnadhimu Mkuu mpya wa Jwtz, Luteni Jenerali Mabeyo,(wapili kulia), katibu Tawala mkoa wa Katavi, Kamishna Paul Chagonja,(wakwanza kulia) na katinu Tawala mkoa wa Mwanza, Kamishna Vlodwin Mtweve (wakwanza kushoto), Mara baada ya hafla ya viapo.
Rais akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Chagonja baada ya kumuapisha


Rais akimuapisha balozi Mahadhi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages