Breaking News

Your Ad Spot

Jan 15, 2016

MUSEVENI USO KWA USO NA HASIMU WAKE MKUU DKT.KIZZA BESIGYE, NI MDAHALO WA KUWANIA URAIS LEO

NA K-VIS MEDIA Na Mashirika ya Habari
RAIS wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, (pichani kushoto), anatarajia kukutana uso kwa uso na hasimu wake mkuu kisiasa, Kanali Dkt. Kizza Besigye, (pichani kulia), kwenye mdahalo wa kuwania urais wa nchi hiyo baadaye leo jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Mdahalo huo unalenga kutoa nafasi kwa wagombea wote wanane wa kiti cha Rais wa Uganda ili wanadi sera zao, watangaze mikakati yao na hatimaye Waganda wawe katika nafasi nzuri ya kuamua nani awe kiongozi wao baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika Februari, mwaka huu 2016
Katika mdahalo huo utakaoongozwa na waandishi wa habari wawili kutoka Kenya raia wa Uganda, Nancy Kacungira na Allan Kasujja
utawaleta pamoja wagombea wengine Sita, akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uganda, John Patrick Amama Mbabazi, Abed Bwanika,  Maureen Kyalya, Venansius Baryamureeba, Joseph Mabirizi na Benon Biraaro.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages