Breaking News

Your Ad Spot

Jan 15, 2016

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

NID1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni (kushoto), akiongozana  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Dickson Maimu (kulia), wakati wa ziara ya kutembelea moja ya ofisi za mamlaka hiyo,iliyopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi,jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri aliweza kupata fursa ya kuangalia jinsi utengenezaji wa kitambulisho cha Utaifa unavyofanyika.


NID2
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni, akiwa katika kikao na viongozi mbalimbali wa Vitengo vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),wakati wa ziara iliyoanzia Makao Makuu ya Mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dickson Maimu.
NID3
Afisa Msajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Emmanuel Joshua(kushoto), akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni(katikati),wakati wa ziara ya Naibu Waziri kwenye mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages