Breaking News

Your Ad Spot

Jan 25, 2016

UGAIDI SI MAFUNDISHO YA UISLAMU

2Sheikh Hemed Jalala akizungumza jambo (aliyekaa) ni mwenyekiti wa taasisi hiyo Sheikh Khalifa Khamis.1Sehemu ya waumini wakifuatilia semina hiyo.

4sehemu ya picha zinazoonesha athari za ugaidi dunianiSehemu ya picha zinazoonesha athari za ugaidi duniani.

Taasisi ya Kiislamu ya Imam Bukhary Muslim Foundation jana ilifanya semina na baadhi ya waumini na wasio waumini wa dini hiyo ili kuujuza umma kuwa ugaidi si mafundisho ya Uslamu kama ambayo wengi wamekuwa wakidhania.

Akizungumza na wanahabari katika katika Hotel ya Lamada, jijini Dar, mwenyekiti wa taasisi hiyo Sheikh Khalifa Khamis amevitaka vyombo vya dola na jamii kuelewa kuwa anapokamatwa mtu kavaa kanzu na anahusishwa na vitendo vya kigaidi asichukuliwe kuwa ni Muislamu bali achukuliewa kama gaidi, Usilamu haufundishi kuuwa watu.

Aidha Kiongozi wa Madhehebu ya Shia nchini, Hemed Jalala alisema wao kama Waislamu wanaupinga vikali ugaidi na jamii nzima inapaswa ifanye hivyo.

“Tunaiomba serikali na jamii nzima itambue kuwa tunapinga vikali vitendo vya ugaidi na wala si mafundisho ya dini yetu kama jinsi ilivyokaririwa, Uislamu hauna sehemu yoyote ile inayofundisha watu wake mafunzo ya kigaidi, mauaji au vitendo vyovyote vile vya kinyama vinavyotendeka duniani,” alisema Jalala.

(Na Gabriel Ng’osha-GPL)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages