IBRAHIM AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA
Katika
kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya
Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa
Septemba 2015.
Mshindi
wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi
zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania
kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya
Simba News.Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group
ambao
ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Richard
Mvula, Ibrahim Ajib alisema “kila siku nimekuwa nikiendelea kujitahidi
kufanya vizuri zaidi ili nami ifike siku niweze kukabidhiwa tunzo hii,
kwakweli ni heshima kubwa sana kwangu, napenda kuchukua fursa hii
kuupongeza uongozi mzima wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia
napenda kuwashukuru mahsbiki wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji
wenzangu kwenye kikosi cha Simba ambao kila siku tumekuwa tukishirikiana
katika kazi yetu hii ya mpira, napenda kushukuru kwa sapoti kubwa
ninayoipaa kutoka kwa familia yangu na mwisho napenda kumshukuru Allah
kwa kuendelea kunibariki na neema zake kila siku”
Akimakabidhi
tunzo hiyo Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group
Richard Mvula alisema “kama mtakumbuka utaratibu huu ulianzishwa kwa
ajili ya kuwapa motisha wachezaji wetu na sasa umekuwa ni utamaduni wetu
katika kuwapongeza na kuonesha kuthamini jitihada zinazofanywa na
wachezaji wetu katika kuutafuta ushindi wa msimu huu”
Napenda
kuwakumbusha wanachama na wapenzi wa Simba kuendelea kuwapa sapoti
wachezaji wetu kwani kwa sapoti yao ndio mafanikio ya timu yetu
yanapopatikana, aliongeza Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka
EAG Group Richard Mvula
Akizungumza
jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG
Group, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda
michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma
jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu
ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza
kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba”.
Tukumbuke
kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na
huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460.
Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa Januari, 2016 litaanza
February 29 2016. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji
wako bora wa Mwezi Januari, 2016.
Simba
News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba
habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya
wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya
Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni
maalum kwa Tigo na Vodacom.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269