SHULE 18 DAR KUNUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUTOKA KWA CFAO MOTORS GROUP NA ALLIANCE AUTOS
Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama
barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika
Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin,
(katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school,
Henning Nathow.
Katika
kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi
jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na
Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada
wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika
Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Akizungumzia
msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa
lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule
ambao wengi wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka barabara.
Alivitaja
vifaa hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha alama za
kusimamisha magari ili wanafunzi wavuke, makoti yanayowatambulisha
waongozaji, kofia za kuwazuia na jua na mipira ya michezo mashuleni na
watatoa elimu katika shule hizo ili kuwasaidia watoto kujua sheria za
barabarani.
“Tumeamua
kutoa msaada huu kwa shule 18 na tutatoa elimu na tutakabidhi vifaa …
tunaamini msaada huu utaweza kuwasaidia watoto hao na tunaamini
itasaidia kupunguza ajali barabarani,” alisema Bi. Tharaia.
Akipokea
vifaa hiyvo kwa niaba ya Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter alisema
wanaishukuru CFAO Motors Group kwa kutambua umuhimu wa elimu na kutoa
vifaa vitakavyoweza kusaidia kuongoza wanafunzi wavukapo barabara.
"Tunashukuru
sana kwa msaada huu na mmeonyesha ni jinsi gani mnatambua umuhimu wa
elimu na sisi tupo pamoja nanyi na tupo tayari kupokea elimu hiyo,"
alisema Bi. Helen.
Alizitaja
baadhi ya shule ambazo zitapata vifaa hivyo kuwa ni Shule ya Msingi
Msimbazi, Boma, Mnazi Mmoja, Uhuru Mchanganyiko, Tabata, Ilala, Lumumba,
Muhimbili, Buguruni, Kasulu, Mkoani, Msimbazi Mseto, Hekima, Amana,
Mtendeni, Buguruni Viziwi na Tabata Jeta na Mtandani.
Pamoja
na hayo pia kunataraji kufanyika mashindano ya mbio za magari yaliyo na
lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya
CFAO Motors Group yanayofanyika nchini na yanataraji kumalizikia nchini
Rwanda.
Meneja
Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah (kulia) akionyesha
baadhi vifaa hivyo vya usalama barabarani kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani).
Mbio
hizo za kusaidia elimu nchini Rwanda zimepewa jina la The go4school
Charity Rally ambazo zimeshirikisha magari 18 ambayo yameanzia jijini
Dar es Salaam na yanataraji kufikia kilele chake Machi, 13 nchini Rwanda
na yatapita katika nchi za Kenya na Uganda na kisha Rwanda.
Akizungumzia
mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin
alisema mbio hizo za magari zimeanzishwa na taasisi ya Volkswagen kwa
kushirikiana na taasisi ya Opportunity International Germany kwa
kutambua kwao umuhimu wa elimu na usalama wa watoto wawapo barabarani.
Alisema
kuwa wamekuwa wakisaidia zaidi katika sekta ya elimu na sio mara ya
kwanza kufanya mbio hizo za magari kwani mwaka 2013 walifanya mbio kama
hizo kutokea Senegal hadi Ghana na mwaka 2015 walifanya kutokea Namibia
hadi Malawi na mara zote kampuni ya CFAO Motors Group imekuwa ikihusika
kufanikisha mbio hizo.
Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya go4school, Henning
Nathow (wa pili kushoto) akielezea dhumuni lengo lao la kusaidia
upatikanaji wa elimu bora kupitia mradi wa go4school.
“Mbio
hizi zimeanzishwa na Wajerumani ili kusaidia elimu ya Rwanda na hii sio
mara ya kwanza tayari yamefanyika mara mbili barani Afrika na sisi
kama CFAO tumekubali kuungana na taasisi ya Opportunity International
Germany ili kusaidia upatikanaji wa elimu,” alisema Potin.
Nae
Henning Nathow ambaye ndiyo mwanzilishi wa mradi wa go4school ulio na
lengo la kusaidia upatikanaji wa elimu bora alisema wanafurahi kufanya
mbiao hizo ambazo zina lengo la kusaidia elimu nchini Rwanda wa
wanaamini elimu ndiyo njia pekee inayoweza kusaidia kupambana na
umasikini.
Alisema
wanataraji kufanya mbio hizo na baada ya kufika Rwanda watayakabidhi
magari yanayotumika kwa ofisi za CFAO za Rwanda na baada ya hapo
watayauza na mapato yatakayopatikana watayakabidhi kwa serikali ya
Rwanda ili kusaidia sekta ya elimu.
“Elimu
ni njia ambayo inaweza kusaidia kumaliza janga la umasikini na sisi
tuna furaha kufanya mbio hizo kuelekea Rwanda ili kusaidia kupatikana
kwa elimu bora Rwanda,” alisema Nathow.
Afisa
Elimu wa Ilala, Helen Peter akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya CFAO
Motors Group kwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani kwa shule
18 zilipo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin (wa pili kushoto) akimkabidhi
Afisa Elimu ya Ufundi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Helen Peter (wa kwanza
kushoto) msaada wa vifaa vya usalama barabarani kusaidia wanafunzi
wavukapo barabarani pamoja na vifaa vya michezo, Wanaoshuhudia tukio
hilo ni Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed na (kulia) na
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Pichani
juu na chini ni kati ya magari 18 yaliyoondoka nchini jana kuelekea
Rwanda kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za magari yaliyo na
lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya CFAO
Motors Group.
Msafara
wa magari aina ya Volkswagen yanayoelekea nchini Rwanda yakitoka kwenye
'showroom' ya Volkswagen iliyopo kampuni ya CFAO Motors Group, barabara
ya Pugu jijini Dar.
KAWAIDA
IMG_4204
Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama
barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika
Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin,
(katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school,
Henning Nathow.
Katika kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za
msingi jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa
kushirikiana na Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen
wametoa msaada wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18
zilizo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Akizungumzia msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed
amesema kuwa lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi
wa shule ambao wengi wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka
barabara.
Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha
alama za kusimamisha magari ili wanafunzi wavuke, makoti
yanayowatambulisha waongozaji, kofia za kuwazuia na jua na mipira ya
michezo mashuleni na watatoa elimu katika shule hizo ili kuwasaidia
watoto kujua sheria za barabarani.
“Tumeamua kutoa msaada huu kwa shule 18 na tutatoa elimu na tutakabidhi
vifaa … tunaamini msaada huu utaweza kuwasaidia watoto hao na tunaamini
itasaidia kupunguza ajali barabarani,” alisema Bi. Tharaia.
Akipokea vifaa hiyvo kwa niaba ya Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter
alisema wanaishukuru CFAO Motors Group kwa kutambua umuhimu wa elimu na
kutoa vifaa vitakavyoweza kusaidia kuongoza wanafunzi wavukapo barabara.
"Tunashukuru sana kwa msaada huu na mmeonyesha ni jinsi gani mnatambua
umuhimu wa elimu na sisi tupo pamoja nanyi na tupo tayari kupokea elimu
hiyo," alisema Bi. Helen.
Alizitaja baadhi ya shule ambazo zitapata vifaa hivyo kuwa ni Shule ya
Msingi Msimbazi, Boma, Mnazi Mmoja, Uhuru Mchanganyiko, Tabata, Ilala,
Lumumba, Muhimbili, Buguruni, Kasulu, Mkoani, Msimbazi Mseto, Hekima,
Amana, Mtendeni, Buguruni Viziwi na Tabata Jeta na Mtandani.
Pamoja na hayo pia kunataraji kufanyika mashindano ya mbio za magari
yaliyo na lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na
kampuni ya CFAO Motors Group yanayofanyika nchini na yanataraji
kumalizikia nchini Rwanda.
Attu Mynah
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah (kulia)
akionyesha baadhi vifaa hivyo vya usalama barabarani kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani).
Mbio hizo za kusaidia elimu nchini Rwanda zimepewa jina la The go4school
Charity Rally ambazo zimeshirikisha magari 18 ambayo yameanzia jijini
Dar es Salaam na yanataraji kufikia kilele chake Machi, 13 nchini Rwanda
na yatapita katika nchi za Kenya na Uganda na kisha Rwanda.
Akizungumzia mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group,
Eric Potin alisema mbio hizo za magari zimeanzishwa na taasisi ya
Volkswagen kwa kushirikiana na taasisi ya Opportunity International
Germany kwa kutambua kwao umuhimu wa elimu na usalama wa watoto wawapo
barabarani.
Alisema kuwa wamekuwa wakisaidia zaidi katika sekta ya elimu na sio mara
ya kwanza kufanya mbio hizo za magari kwani mwaka 2013 walifanya mbio
kama hizo kutokea Senegal hadi Ghana na mwaka 2015 walifanya kutokea
Namibia hadi Malawi na mara zote kampuni ya CFAO Motors Group imekuwa
ikihusika kufanikisha mbio hizo.
Henning Nathow
Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya go4school, Henning Nathow
(wa pili kushoto) akielezea dhumuni lengo lao la kusaidia upatikanaji
wa elimu bora kupitia mradi wa go4school.
“Mbio hizi zimeanzishwa na Wajerumani ili kusaidia elimu ya Rwanda na
hii sio mara ya kwanza tayari yamefanyika mara mbili barani Afrika na
sisi kama CFAO tumekubali kuungana na taasisi ya Opportunity
International Germany ili kusaidia upatikanaji wa elimu,” alisema Potin.
Nae Henning Nathow ambaye ndiyo mwanzilishi wa mradi wa go4school ulio
na lengo la kusaidia upatikanaji wa elimu bora alisema wanafurahi
kufanya mbiao hizo ambazo zina lengo la kusaidia elimu nchini Rwanda wa
wanaamini elimu ndiyo njia pekee inayoweza kusaidia kupambana na
umasikini.
Alisema wanataraji kufanya mbio hizo na baada ya kufika Rwanda
watayakabidhi magari yanayotumika kwa ofisi za CFAO za Rwanda na baada
ya hapo watayauza na mapato yatakayopatikana watayakabidhi kwa serikali
ya Rwanda ili kusaidia sekta ya elimu.
“Elimu ni njia ambayo inaweza kusaidia kumaliza janga la umasikini na
sisi tuna furaha kufanya mbio hizo kuelekea Rwanda ili kusaidia
kupatikana kwa elimu bora Rwanda,” alisema Nathow.
Helen Peter
Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya
CFAO Motors Group kwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani kwa
shule 18 zilipo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Eric Potin
Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin (wa pili kushoto)
akimkabidhi Afisa Elimu ya Ufundi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Helen Peter
(wa kwanza kushoto) msaada wa vifaa vya usalama barabarani kusaidia
wanafunzi wavukapo barabarani pamoja na vifaa vya michezo, Wanaoshuhudia
tukio hilo ni Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed na (kulia)
na Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah.
Eric Potin
Attu Mynah
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Volkswagen Tanzania
Pichani juu na chini ni kati ya magari 18 yaliyoondoka nchini jana
kuelekea Rwanda kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za magari
yaliyo na lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na
kampuni ya CFAO Motors Group.
Volkswagen, Tanzania
IMG_4332
Msafara wa magari aina ya Volkswagen yanayoelekea nchini Rwanda yakitoka
kwenye 'showroom' ya Volkswagen iliyopo kampuni ya CFAO Motors Group,
barabara ya Pugu jijini Dar.
Volkswagen Tanzania
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269