Breaking News

Your Ad Spot

Feb 27, 2016

 Rais mstaafu wa awamuya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akipungia mamia ya wapenzi wa mchezo wa kikapu, wakati akipokewa na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde, kwenye kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK), kilichoko Kidongo Chakundu Kariakoo jijiniDar es Salaam, Februari 27, 2016. JK alikwenda kuzindua ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana.(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
RAIS mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezindua mashindano ya ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana yaliyopewa jina NBA Junior kwenye kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK-Park), kilichoko Kidongo- Chekundu, Kariakoo jijini Dar es Salaam, Februari 27, 2016.
Rais alitoa hotuba na kisha kuzindua mashindano hayo kwa kutumbukiza mpira kwenye goli (kikapu), na hivyo kuthibitisha maneno yake kwenye hotuba kuwa yeye alikuwa mpenzi mkubwa wa mpira wa kikapu.
Gwiji wa ligiya WNBA huko Marekani, Allison Feaster ambaye alikuwa ni miongoni mwa wasemaji wakuu kwenye uzinduzi huo, alifurahi mno kwa kupiga makofi na kasha kugongesha mikono na Dkt. Kikwete.
Miongoni mwa wasemaji wakuu wengine ni pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa kampuni ya kufua umeme ya Kimarekani, Symbio, Paul Hinks. Symbion ndio waliojenga kituo hicho. Lakini pia Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa NBA kanda ya Afrika, Amadou Gallo Fall, pia alihutubia kwenye uzinduzi huo.
Serikali iliwakilishwa na naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde.
Pia Mbunge wa Ilala, sehemu kilipo kituo hicho, Mussa Azzan Zungu alikuwepo
Ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana (NBA Jr), ni ligi ya kidunia yenye program maalum kwa wavulana na wasichana, inafundisha stadi za msingi pamoja na maadili ya msingi katika hatua za mwanzo kabisa kama jitihada za kukuza nakuboresha uzoefu wa wachezaji, makocha na wazazi kwenye mpira wa kikapu.
Kama ilivyo kwenye ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani (NBA), timu 30 zimegawanywa kwenye makundi mawili na daraja sita. Timu bora nane kutoka kila kundi zitafuzu kushiriki kwenye ngazi ya mtoano Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi (Ukanda), zitakutana kwenye michezo ya kuwania ubingwa ili kumpata bingwa wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana iliyofanyika kwa mara ya kwanza






 JK akitoa hotuba yake ya uzinduzi
 Afia Mtendaji Mkuu (CEO) wa Symbio Power, Paul Hinks, akizungumza kwenye uzinduzi huo
 Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa NBA kanda ya Afrika, Amadou Gallo Fall, akizungumza
 Gwiji wa mchezo wa Mpira wa kikapu kwenye ligi ya WNBA ya Marekani,
Allison Feast, akizungumza kwenye uzinduzi huo


 JK, akiomba mpira autumbukize kimianihuku akiongozana na gwiji huyo wa mpira wa kikapu Marekani, Allison Feast
 Allison Feast alishangilia kwa kupiga makofi baada ya JK kuutumbukiza kimiani mpira huo akiwa umbali wa mita 3 kutoka kwenye mlingoti wa goli
 Rashidi Kikwete, mtoto wa JK, akifurahia baada ya baba yake kuuweka mpira kimiani. Rashidi naye ni mpenzi mkubwa wa mchezo huo na huenda akawa nyota hapo baadaye
 "Hebu nipe tano" ndivyo anavyoonekana kusema Allison akigongesha mkonona JK baada ya Rais huyo mstaafu kuonyesha umahiri wake kwenye mcehzo wa mpira wa kikapu kwa kufunga goli akiwa umbali wa takriban mita tatu kutoka kwenye mlingoti








 JKakiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto, Rais wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, John Bandiye, Mbunge wa Ilala, MussaAzzan Zungu, Hinks, JK, Amadou Gallo Fall, Naibu Waziri Mvunde, na Allison Feast
 JK akiteta jambo na naibu waziri Mavunde
 Allison akiwapasha waandishi wa habari
 Timu za Chicago (waliovaa nyekundu) ambao kwa jina lao halisi ni Shule ya msingi Juhudi ya hapa jijini Dar es Salaam kule Ukonga, na waliovaa kijani ni Celtic kwa jila lao halisi ni shule ya msingi UN-Muhimbili ya Upanga jijiniDar es Salaam, wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mtanange
 Picha ya kumbukumbu, naibu waziri Mavunde, akiwa katka picha ya pamoja na mkuu wa skauti jijini Dar es Salaam, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Mafia, Abdulkarim Sha (kulia) na skati mwanadada
JK akipena mikono na Allison wakati akiwasili JMK Park

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages