Breaking News

Your Ad Spot

Feb 17, 2016

KATIBU MUU WA ZAMANI WA UN AFARIKI DUNIA

Katibu Mkuu wa zamani wa UN afariki dunia
Mwanasiasa wa Misri Boutros Boutros-Ghali aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 1992 hadi 1996 amefariki dunia.
Boutros Boutros-Ghali alifariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 94.
Rafael Ramires, mwanadiplomasia wa Venezuela ambaye ndiye rais wa sasa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alitangaza jana habari hiyo katika kikao cha baraza hilo kilichokuwa kikijadili suala la Yemen na kutaka hadhirina wanyamaze kimya dakika moja kwa mnasaba wa kufariki dunia mwanasiasa huyo mkongwe wa Misri.
Katika kipindi cha uongozi wake kwenye Umoja wa Mataifa, Boutros Boutros-Ghali alichukua hatua za kufanyia marekebisho muundo wa sekretarieti ya umoja huo na kupanua zaidi maana ya operesheni za mapema kwa ajili ya kulinda amani duniani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages