MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUTAFUTA WAWAKILISHI WA NCHI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR’AN TUKUFU.
Makamu wa Rais mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya
kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye
mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu, yaliyoandaliwa na Kamati
Maalum chini ya Mwenyekiti wake Saleh Omary, yaliyofanyika kwenye Ukumbi
wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Picha na Mafoto
Blog
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi
zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi
atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan
Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati
wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati
maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. . Kushoto ni Balozi wa
Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar . Picha na Mafoto Blog
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi
zawadi, mshindi wa pili wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi
atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan
Tukufu, Ibrahim Omary, aliyepata pointi 90 kwa upande wa Tajweed, wakati
wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati
maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran
nchini Tanzania, Mahd Aghajafar. Picha na Mafoto Blog
Baadhi ya waumini wa dini ya
kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal,
wakati akihutubia. Picha na Mafoto Blog
Baadhi ya waumini wa dini ya
kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal,
wakati akihutubia. Picha na Mafoto Blog
Makamu wa Rais Mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea
zawadi kutoka kwa Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar, wakati
wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha
Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu hayo
yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb
28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya
Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Al-had Mussa Salum. Picha na Mafoto Blog
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi
ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mashindano ya
kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye
mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan Tukufu. Picha na Mafoto Blog
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Sl-had Mussa Salum, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi, kufunga mashindano hayo. Picha na Mafoto Blog
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo,Saleh Omary, akizungumza wakati wa mashindano hayo. Picha na Mafoto Blog









No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269