Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amempongeza Theophil Makunga kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mwishoni mwa wiki.
Katika
salamu hizo, Malinzi amempongeza Makunga kwa nafasi hiyo aliochaguliwa
na kusema imani waliyonayo wahariri wenzake juu ya utendaji wake wa kazi
ndio kumepelekea wao kumchagua kuongoza jukwa hilo.
Aidha
Malinzi amewapongeza Deodatus Balile aliyechaguliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti na Neville Meena aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa
hilo na kuahidi kuwa TFF itaendelea kushirikiana nao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269