Breaking News

Your Ad Spot

Feb 13, 2016

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAZEE WA DAR ES SALAAM, ASKOFU GWAJIMA NDANI

1
Rais Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee tayari kwa kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo ambapo mkutano huo pia ulihudhuriwa na Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amehudhuria katika mkutano huo ambapo alionekana mtu mwenye kufurahia hotuba hiyo, Kamera ya Fullshangwe ilimnasa askofu huyo maarufu kwa matamshi yake ya “Wakale Malimao”  akiwa na tabasam kubwa  akionekana kufurahia kuhudhuria kwake katika mkutano huo.
Mwanzo wakati alipofika ukumbini hapo alikuta  ratiba inaendelea hivyo ilibidi akae viti vya nyuma lakini Shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim alimpigia simu na kumwambia aende mbele akakae pamoja na viongozi wenzake wa dini na ndipo alipoenda kukaa eneo hilo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Msafara wa Rais Dk. John Magufuli ukiwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
3
Rais Dk. John  Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es salaam mzee Hemed Mkali kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.
4
Rais Dk. John  Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es salaam wa zamani Mzee Idd Simba, Kulia ni mfanyabiashara Abdullah Mohamed.
5
Rais  Dk. John Magufuli akiteta jambo na Waziri Mkuu  Majaliwa Kassim Majaliwa.
6
Rais  Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na Mke wa Rais Mama Janet Magufuli  wakiwa meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam.
7
Baadhi ya mawaziri wa wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya tano wakiwa katika mkutano huo.
8
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo na ya Kiislamu wanaounda kamati ya Amani wakiwa katika mkutano huo
15
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hakubaki nyuma na yeye amehudhuria katika mkutano huo na hapa akionekana mwenye furaha na bashasha kama alivyonaswa na kamera yetu.
06
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amekaa pamoja na viongozi wenzake wa dini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam wakati Rais Dk. Magufuli alipozungumza na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
9
Baadhi ya wazee wa Dar es salaam wakitambulishwa katika mkutano huo.
11
Baadhi ya mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo kutoka kulia ni Profesa Sospeter Muhongo, Dk. Abdallah Posi, Nape Nnauye, Januari Makamba na Ummy Mwalimu.
12
Baadhi ya wazee wakifuatilia kwa makini wakati Rais  Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano huo.
13 14
16
Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimia wazee katika mkutano huo.
17
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wazee katika mkutano huo.
18
Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es alaam Mzee Hemed Mkali akihutubia katika mkutano huo na kumkaribisha Rais Dk.  Magufuli ili kuwahutubia wazee hao.
19
Wazee hawa wakionekana kuhamasika na hotuba ya Rais Dk. Magufuli.
20
Rais Dk.  Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages