Mtambuzi
wa miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijini, Mhandisi Elneema Mkumbo
akitoa maelezo juu ya utekelezaji wa miradi ya REA, kwa Mkuu wa Shirika
la Kimataifa la Maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlokom (
aliyeweka mikono kifuania) ambao ni miongoni mwa wafadhili wa miradi
hiyo akiwa na ujumbe wake pamoja na wadau wengine wa maendeleo ikiwemo
Shirika la Maendeleo la Ujerumani( GIZ) wakati wakikagua utekelezaji wa
miradi ya REA katika mikoa ya kanda ya kaskazini.
Muonekano
wa nyumba zilizounganishwa na huduma ya umeme unaotekelezwa na Wakala
wa Nishati vijijini REA katika kijiji cha Kwedizinga mkoani Tanga.
……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Shirika
la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA), limeridhishwa na
utekelezaji wa miradi ya Umeme inayofahiliwa na Shirika hilo hususan
usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini
REA kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini( Tanesco), katika
maeneo mbalimbali nchini.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlekom amesema hayo mara baada ya
kuona maendeleo ya wananchi wa vijijini wakati wa ziara yake ya
kutembelea utekelezaji wa miradi hiyo katika mikoa ya kanda ya kaskazini
.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269