Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga enzi za uhai wake.
AFISA Uhusiano
wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga,
amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 27, 2016.
Taarifa ya kifo cha Bi. Amanda imethibitishwa na Meneja Uhusiano wa
TTCL, Bw. Nicodemus Thom Mushi.
"...Ni
kweli, Bi Amanda amefikwa na umauti akiwa likizoni mkoani Mbeya
alikokwenda kuwasalimu ndugu zake.. Aliugua ghafla Alhamisi hii na
kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi usiku wa kuamkia Jumamosi
ambapo Mungu alimchukua," alisema Bw. Thom Mushi.
Alifafanua
kuwa mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Jumapili, kutoka Mbeya
kwenda Njombe na Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu tar
29.02.2016 katika Kijiji cha Mlangali, Ludewa, Mkoa wa Njombe. Mtandao
huu unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Bi.
Amanda Fredrick Luhanga kwa msiba mkubwa uliowafika. Bwana alitoa,
Bwana ametwaa, Apumzike kwa Amani |
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269