Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa
habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa
Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini
Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya
Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa
Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa
Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa
habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa
habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean
View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni
orijinali unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06# na
utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15 mfano
IMEI 12456789067654 Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu
yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY
C5555 - Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa
Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa
waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa
hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269