Baba akiwa amembeba mwanaye aliyezaliwa akiwa ameathirika na Virusi vya ZIKA huko Brazil
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
UGONJWA
wa ZIKA unaoenezwa na virusi vya microcephaly vinavyotoka
kwenye Mbu, umetangazwa kuwa ni janga la kimataifa.
Maambukizi
ya ZIKA ambayo wataalamu wanahofia kuwa vinasambaa kwa kasi na kuhusishwa na
maelfu ya watoto waliozaliwa na udhaifu wa kukua kwa ubongo na hivyo kuathiri
ukuaji wa viungo vya mwili.
Tangazo
la Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), limeuweka ugonjwa huu kwenye kundi la
magonjwa hatari kama EBOLA na itasaidia utafiti ambao utapelekea kupambana na
maambukizi..
Tayari
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuwa Tanzania
hakuna tishio la ugonjwa huo lakini akawataka wananchi kuchukua tahadhari na
kutoa taarifa mara waonapo motto anazaliwa akiwa na maumbileyasiyo ya kawaida.
Virusi
hivi humshambulia mama mjamzito aliyeng’atwa na Mbu mwenye virusi hivyo na
hupelekea kuzaa mtotomwenye kicwa kidogo na ubongo mdogo.
Mkuu
wa WHO, Margaret Chan, amesema katika tangazo lake kuwa kuna uhusiano mkubwa
kati ya vimelea vya ZIKA na microcephaly kuwa ndio vimesababisha janga hilo
ingawa bado haijathibitishwa kisayansi.
Ugonjwa
wa ZIKA umesambaa sana kwenye nchi za Marekani Kusini hususan Brazil
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269