Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea nakala yake ya
fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kutoka kwa Kamishina wa
Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye
Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambako ilitiwa saini na kamishina
huyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es
salaam Februari 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambao walikwenda ofisini kwake
jijini Dar es salaam Februari 15, 2016 kumpatia nakala yake ya fomu ya
ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma ambayo aliitia saini na kuipeleka
kwenye Secretarieti hiyo ambako ilitiwa saini na Kamishina wa Maadili,
Jaji Mstaafu Salome Kaganda (wapili kulia).Kushoto ni Katibu wa Idara ya
Viongozi Watumishi wa Umma, Secretarieti ya Maadili , John Kaole na kulia ni
Katibu wa Idara ya Viongozi wa Siasa, Secretariet ya Maadili ya Viongozi wa
Umma, Waziri Kipacha.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269