UGANDA imetengeneza basi la abiria
linalotumia nguvu ya jua kufanya kazi.
Rai wa Uganda Paul Isaac Musasizi ndiye
aliyebuni basi hilo na sasa liko tayari kwa safari na litazinduliwa rasmi
Jumanne Februari 16, 2016.
Basi hilo litakuwa ni la kwanza la aina
yake kubuniwa barani Afrika na kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, basi
hilo lina uwezo wa kubeba abiria 35 na litakuwa na uwezo wa kutembea
Kijana huyo ambaye ndiye Afisa Mtendaji
Mkuu, (CEO) wa kampuni ya Kiira Motors Corporation, amesema kwa vile Uganda wanapata jua
siku zote, ndiyo maana aliona abuni basi litakaloendeshwa na nguvu ya jua
(Solar Powered electric bus).
Mvumbuzi huyo alisema, basi hilo
limepewa jina la kilugha “Kayoola” lina uwezo wa kusafiri maili 50 bila
kusimama likitumia betri mbili moja likiwa limeunganishwa na kifyonja mionzi ya
jua (Solar Panels), kilichofungwa juu ya basi, na betri nyingine hujichaji kwa
safari ndefu hususan wakati wa usiku.
RaisYoweri Museveni anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo wa kesho na sasa “Kayoola” ambayo ilifanyiwa
majaribio kwenye mitaa ya Kampala na jirani na uwanja wa taifa ndio habari ya
mujini.
![]() |
| Wafanyakazi wa kampuni ya Kiira Motors Corporation, wakitazama michoro ya basi hilo wakati wa hatua za mwanzo za kulibuni |



No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269