Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuchukuliwa hatua
kali dhidi ya askari wa kulinda amani wa kimataifa waliohusishwa na
vitendo vya kunajisi wanawake.
Ban Ki-moon ambaye jana alikuwa akihutubia Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa mjini New York alisema kuwa, askari walionajisi na
kubaka wanawake wanapaswa kupandishwa kizimbani na kuhukumiwa.
Wito huo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa umetolewa baada ya
kukithiri vitendo viovu kama hivyo vya askari wa kimataifa wa kilinda
amani katika nchi mbalimbali hususan huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Baadhi ya nchi pia zinatuhumiwa kuwa hazichukui hatua za kutosha dhidi
ya askari wao waliohusishwa na vitendo viovu vya kunajisi au kutumia
vibaya wanawake wakiwa katika majukumu yao ya kulinda amani.
Nchi kadhaa wanachama wa Umoja wa Mataifa zimependekeza muswada
katika Baraza la Usalama la umoja huo zikitaka kurudishwa nyumbani
askari wote wanaotuhumiwa kubaka wanawake au kuhusika na ukatili wa
kingono.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269