Breaking News

Your Ad Spot

Mar 22, 2016

CHADEMA WASHINDA UMEYA WA JIJI LA DAR ES ASALAAM, LEO

Na Anita Jonas-Maelezo
Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Jiji la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Diwani wa Kata ya Vijibweni, Manispaa ya Temeke (CHADEMA), Isaya Chacha Diwani kuwa Meya Mpya wa Jiji hilo.

Kaimu Mkurugenzi huyo alimtangaza Isaya kuwa mshindi mwishoni mwa uchaguzi uliofanyika leo, na diwani huyo kuibuka mshindi kwa kupata kura 84 dhidi ya mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67 wakati kura 7 ziliharibika katika uchaguzi huo.

 “Tunawashuruku wapiga kura wote mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza kufanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili” alisema Bi Yohana.

Kwa upande wa mshindi wa Kiti cha Meya wa Jiji Mhe. Chacha aliwashukuru wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho cha Umeya.

“Nimejipanga kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji letu na nitahakikisha wananchi wote maskini wanafaidika  na mapato ya jiji hili ikiwemo kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages