Naibu
wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha
hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini
kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa
kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa
kuwa.
Dk.
Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya
ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu
mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna
ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye
chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt.
Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo
utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.
“Chumba
cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko
chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia
mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa
maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.
Aidha
uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo
ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake
pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.
Katika
ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi
hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa
mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.
Dkt.
Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa
chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum
zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha
mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa
vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya
vifaa vinavyotumika.
Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.
Kwa
upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale
yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.
Tazama MO tv, kuangalia tukio hilo hapa:
Imeandaliwa na Magreth Kinabo, (MAELEZO), Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv)
Naibu
wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja
uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati
walipowasilia katika ziara hiyo..
Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
Dk.
Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna
Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa
ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa
Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
Dk.
Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe
mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..
Dk
Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha ya
kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri
unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi
Naibu
Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi
pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa
ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za
Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote
na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).
KAWAIDA
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji
cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya
kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake
kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho
kinavyotakiwa kuwa.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016,
alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane
na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia
namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo
kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi,
Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo
utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.
“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki
kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia
mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa
maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.
Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha
maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi
wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa
watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo
kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.
Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa
kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama
maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba
cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia
vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una
idadi ya vifaa vinavyotumika.
Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale
yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.
Tazama MO tv, kuangalia tukio hilo hapa:
Inline image 1
Imeandaliwa na Magreth Kinabo, (MAELEZO), Andrew Chale, Modewjiblog/MO
tv)
dk kigwa
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa
Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati
walipowasilia katika ziara hiyo..
dk hk 888Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali
hiyo.
dk hk55Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo
pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia
haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua
ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora
anayostahiki.
Kigwangalla akitoa maagizo
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali
hiyo, Bi. Gean Cabral
dk hkna
Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe
mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
dk kigwa
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo
pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..
dk hk iio
Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha
ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri
unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi
dk hk67
Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali
Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya
kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji
katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu
binafsi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269