
Hivi Karibuni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilirusha angani kwa
mafanikio makombora kadhaa ya balistiki ikiwa ni katika kuyafanyia
majaribio.
Luteka hiyo ya makombora ambayo inasisitiza udharura wa
kuonyeshwa nguvu ya kuzuia kufanyika makosa ya adui na kujitayarisha
Iran ya Kiislamu katika pande zote kwa ajili ya kukabiliana na kila
aina ya vitisho dhidi ya Mapinduzi, Mfumo na ardhi yote ya Iran,
imefanmyika katika hatua kadhaa. Kamanda mkuu wa Jeshi la Walinzi wa
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC alisisitiza siku ya Jumanne mwishoni
mwa luteka hiyo iliyopewa jina la "Nguvu ya Wilaya' kwamba kila mtu
anayeifanyia uadui zaidi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bila shaka ndiye
anayepaswa kuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na uwezo na kujitayarisha
Iran katika uwanja huo. Majaribio hayo ya makombora ya Iran yametajwa na
baadhi ya watu kuwa tishio kwa usalama. Josh Earnest Msemaji wa White
House katika matamshi yake ya kila siku mbele ya waandishi habari
ameashiria Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kusema
kuwa licha ya kuwa majaribio hayo hayakiuki mapatano ya mpango huo
lakini serikali ya Washington inachunguza iwapo suala hilo linapasa
kuchunguzwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa au la.
Peter Cook, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani pia amesema kuwa
majaribio hayo ya makombora ya Iran yanatia wasiwasi na kudai kuwa
yanakiuka maazimio ya Baraza la Usalama.
Kwa mujibu wa azimio nambari 1929 lililopasishwa na Baraza la Usalama
mwezi Juni 2010 Iran iliizuiwa kufanya majaribio yoyote ya makombora ya
balistiki, lakini azimio jipya nambari 2231 lililopasishwa na baraza
hilo mwezi Julai mwaka uliopita, baada ya kufikiwa mapatano ya nyuklia
kati ya Iran na kundi la 5+1 mashuhuri kwa ufupisho wa JCPOA, maazimio
yote ya hapo kabla ya baraza hilo dhidi ya Iran yalifutwa. Katika azimio
hilo jipya Iran iliombwa kutotengeneza makombora yaliyo na uwezo wa
kubeba vichwa vya nyuklia, katika kipindi cha utekelezaji wa mpango wa
JCPOA. Hivi sasa inadaiwa kuwa makombora ya Iran yana uwezo wa kubeba
vichwa vya aina mbili yaani vya kawaida na vya nyuklia. Hii ni katika
hali ambayo Iran haina makombora yaliyotengenezwa kwa ajili ya kubeba
vichwa vya nyuklia. Hata kabla ya kutiwa saini mapatano ya JCPOA, Iran
ilitangaza wazi kwamba makombora ya kujilinda ya Iran si suiala
linaloweza kujadiliwa na kwamba haijawahi kufanya mazungumzo na Marekani
au upande wowote ule kuhusiana na kadhia hii. Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran imetangaza wazi kupitia viongozi wake wa ngazi za juu kwamba silaha
za nyuklia hazina nafasi katika mfumo wake wa ulinzi. Pia hakuna wakati
wowote ambapo makombora ya Iran yametengenezwa kwa ajili ya kubeba
vichwa vya nyuklia wala majario yoyote kufanyika katika uwanja huo. Kwa
maelezo hayo, uwezo wa kujilinda wa makombora ya Iran si tu kwamba sio
tishio kwa usalama wa wengine bali ni nguvu ya kuzuia maadui kufanya
makosa ya kihujuma, na hilo ni kwa maslahi ya usalama wa eneo la
Mashariki ya Kati na ulimwengu mzima kwa jumla. Ni wazi kuwa Wamarekani
wanaeneza propaganda dhidi ya makombora ya Iran ili waweze kuendeleza
mpango wao wa kuidhihirisha Iran kuwa tishio kwa usalama wa eneo.
Marekani imekuwa ikitumia masuala matatu ya uwezo wa makombora ya Iran,
haki za binadamu na demokrasia, kama visingizio vya kuzidisha
mashinikizo dhidi ya Iran. Jambo hili linabainisha wazi kwamba Marekani
ingali inatumia madai yasiyo na msingi ili kudumisha uadui wake wa muda
mrefu dhidi ya Iran.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269