
Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
anayeshughulikia masuala ya Kiarabu na Kiafrika amesema kuwa,mgogoro wa
Syria unapaswa kutatuliwa kwa kuheshimu ardhi yote, mamlaka na umoja wa
kitaifa wa nchi hiyo ya Kiarabu.
Hossein Amir Abdollahiyan amesema hayo katika mazungumzo yake kwa
njia ya simu na Staffan de Mistura mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria na kusisitiza juu ya udharura
wa kutazama mambo kwa uhalisia wake katika kufuatilia suala la kupambana
na ugaidi na mwenendo wa kisiasa katika nchi hiyo ya Kiarabu. Naibu
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
anayeshughulikia masuala ya Kiarabu na Kiafrika amesisitiza kuwa, kuna
haja ya kuwa macho na hatua ambazo zinapelekea kuyaimarisha makundi ya
kigaidi.
Kwa upande wake Staffan de Mistura mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria ameashiria katika mazungumzo
yake na Hossein Amir Abdollahiyan juu ya nafasi muhimu na athirifu ya
Iran katika kuupatia ufumbuzi wa kisiasa mgogoro wa Syria na kuelezea
azma ya kweli ya Umoja wa Mataifa katika kufuatilia kadhia ya mgogoro wa
nchi hiyo ya Kiarabu.
Wakati huo huo de Mistura amesema mazungumzo kuhusu Syria
yanayotarajiwa kuanza Jumatatu huko Geneva, Uswisi hayataangazia masuala
ya kibinadamu na sitisho la mapigano. Akizungumza na waandishi wa
habari Jumatano baada ya mkutano wa kikundi cha kimataifa cha usaidizi
wa Syria, ISSG, de Misturra amesema badala yake ajenda zitakuwa ni uongozi
mpya, katiba na uchaguzi, yaani chaguzi zijazo katika miezi 18 ijayo za
Rais na wabunge. Masuala ya sitisho la mapigano kinadharia na kivitendo
tunaamini hayapaswi kujadiliwa kwenye mazungumzo hayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269