Breaking News

Your Ad Spot

Mar 16, 2016

MAKONDA AANZA KAZI, AWAPA SAA 24 WAKURUGENZI NA WAKUU WA VITENGO KUMPATIA CHANGAMOTO ZIPATIWE UFUMBUZI

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwasili kwa mara ya kwanza ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana.
 Katibu Tawala Msaidizi- Utawala, Ellha Mcha (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumpokea rasmi jana alipofika kwa mara ya kwanza katika ofisi yake.
 Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shabani Mhando akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 Mkurugenzi mpya wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli akisalimiana na Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kushoto), akizungumza wakati wa kumakribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na RC Paul Makonda.
Wakuu wa Idara mbalimbali katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye hafla ya kumpokea mkuu wao wa mkoa.
 Mkutano ukiendelea.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, akimkabidhi kadi ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali katika ofisi yake.


Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza kazi rasmi leo kwa kuzungumza na wakuu wa idara na Vitengo na kutoa maagizo mazito kwa kuwapa viongozi hao saa 24  wawe wamempa taarifa zilizopo katika maeneo yao husika zenye kuelezea changamoto ili zipatiwe ufumbuzi.

Mbali na wakuu hao wa Idara na vitengo, mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, pia walihudhuria Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wakurugenzi na Makatibu Tawala wa wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam. 

Awali Makonda alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanikisha yeye kushika nafasi hiyo baada ya Mheshiwa Rais Dk.John Magufuli kusikia sauti ya Mungu na kuifanyia kazi ya kumchagua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Makonda alimshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kushika nyazifa hiyo muhimu ya kuwatumikia wananchi ambapo pia alimshukuru Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam wa zamani, Saidi Meck Sadiki kwa kumpokea akiwa kama Mkuu wa Wilaya na kumfundisha mambo mengi makubwa na mazuri ambayo yamemfanya kwa namna moja au nyingine kupata nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa.

Makonda amesema kwamba kwa sasa hajui chochote badala yake amewaomba watendaji wote kuonesha ushirikiano kati yao ili kuupeleka kwa kasi mkoa wa Dar es Salaam kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages