Breaking News

Your Ad Spot

Mar 22, 2016

MBUNGE VITI MAALUMU ASAIDIA AKINA MAMA WAJASILIAMALI.

 Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve
 Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve akiwana baadhi ya wananchama wa chama ch mapinduzi.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Sebastian Emmanuel jr. Mafinga.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve ameendelea kukutana na makundi mbalimbali katika mkoa
huo, mwishoni mwa wiki hili amekutana na wajasiliamali wanawake katika makundi
mawili tofauti. Kundi la kwanza alilokutana nalo ni lile la umoja wa wanawake
wa ccm Iringa mjini, waliounda vicoba kwa ajili ya kukopeshana na kuendeleza
miradi kadhaa ya kijasiliamali.
Aidha wanawake hao wakati wakisoma risala kwa mbunge huyo wamesema kuwa wanakabiliana na changamoto kadhaa hasa
ukosefu wa mtaji utakao wafanya waendeleze vicoba hivyo ambavyo imekuwa
kimbilio la makundi mbalimbali mijini na vijijini.
Pia wanawake wao wamemwomba mbunge huyo kuhakikisha kuwa wanawake wa mkoa wa Iringa wanakuwa mfano wa kuigwa
katika kuanzisha, kukilinda na kukitetea chama chao hicho cha vicoba kwa kuwa
vinaonesha nia ya kuwasaidia kujikimu kimaisha, mpaka sasa wameanza kutafuta
wataalamu wa kufundisha namna ya kufuga kuku ili wapate elimu sahihi na kasha kuanza
kutekeleza mladi huo.
Kwa upande wake mbunge huyo kijana ametoa milioni moja taslimu kama mkopo usiokuwa na riba ili uweze kuwasaidia
kuendeleza mtaji wao pia akatumia fursa hiyo kuwaomba mkopo huo wauzungushe
katika miradi mbalimbali kama ya ufugaji kuku n.k. pia ameonesha nia ya
kuwasaidia wanawake hao na kuwaahidi kuwa wakiwa na uaminifu wa kulinda mtaji
wao hata kama ni mdogo atahakikisha kuwa vicoba hiyo inakuwa ya mfano wa kuigwa
mkoani Iringa. 
Mbunge huyo amewaomba wanawake wote wa mkoa wa Iringa wasikate tamaa badala yake wapende kujifunza na kutaka
kupata nafasi ambayo itawapeleka kwenye mwanga wa  mafanikio. Amesema kuwa hata yeye amekuwa
akithubutu kujituma kwa bidii ili aweze kufikia lengo la kuwasaidia wanawake
wote bila kujali itikadi, kabila wala dini zao.
Aidha kundi jingine la pili ni lilela wanawake wanaoishi na ulevu Mjini Iringa, wametumia fursa hiyo kuongea
na mbunge huyo na kumweleza changamoto wanazokumbana nazo, ikiwa ni pamoja na
kutokuwa na mtu wa kuwasaidia kwa mda mrefu kulingana na changamoto zinazo
wakabili na kuonesha imani kwa mbunge huyo kuwa sasa wanamatumaini mapya kuwa
wamepata mtu muafaka wa kuwasaidia.
Wanawake hao wanaoishi na ulemavu wameomba pia kupatiwa mtaji ili uweze kuwasaidia katika umoja wao wa kazi za
mikono ikiwa ni ususi wa shanga za kimasai, mikoba ya kimasai na mikoba ya
kisasa kwa kutumia shanga mbalimbali za asili, ambapo mbunge huyo licha ya
kuwapa kiasi cha pesa kwa ajili ya kuendeleza mtaji wao pia amewaomba waanzishe
mladi wa utengenezaji wa batiki utakao wanufaisha kwa kiwango kikubwa kwani
unaonesha kuwa na soko la uhakika.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages