Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Jijini Mwanza, Joseph Stanford,
maarufu kwa jina la Rich4D akiwaonyesha wanahabari Jijini Mwanza (hawapo
pichani) ramani ya Mkoa wa Dar es salaam aliyoitumia kutambua maeneo ya
Mkoani huo.
Hiyo
ilikuwa baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuonana na
Rais John Pombe Magufuli ili kumpongeza kwa kuwajumuisha wasanii katika
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika baraza lake la
Mawaziri. Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kutimiza adhma yake hiyo.
Msanii
Joseph Starnford maarufu kwa jina la Rich4D alitembea kwa miguu kutoka
Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kumpongeza Rais John
Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Baraza lake la Mawaziri,
amesisitiza kuwa shauku yake ni kuonana na rais ili kutimiza adhma yake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269